Quantcast
Channel: ARTS AND CULTURE IN TANZANIA
Viewing all 51 articles
Browse latest View live

Vyama vya wasanii Tanzania

$
0
0
Katika kitendawili kinachoendelea katika tasnia ya muziki ni swala la vyama vya wasanii. Kuna aina nyingi ya vyama, vya kitaaluma kama vile Chama cha wapiga bezi au cha wapiga trumpet, vyama vya aina za muziki, kwa mfano muziki wa dansi, taarab, hiphop na kadhalika kisha vyama vya haki mbalimbali katika hakimiliki, vyama vya haki za wanamuziki kama wafanya kazi na kadhalika. Kumekuwa na mkanganyiko wa vyama kuanzishwa na kuwa vinafanya kazi nyingi kwa pamoja  hivyo hatimae kujikuta vikishindwa kazi. Tatizo jingine ni uelewa mfinyu wa wasanii kuhusu haki zao na hivyo kutokuona umuhimu wa kujiunga na chama chochote au kudhani vyam ni vingi mno kwa mtu mmoja. Wafanyabiashara wasiowaaminifu wamekuwa wakiwakataza wanamuziki kujiunga kwa kuwa wanajua umoja ni nguvu.

Kamatakamata ya Alex Msama, mfano wa kuigwa

$
0
0

Katika wiki za karibuni kumekuweko na jitihada za kipekee za Alex Msama na kampuni yake kufanya kamatakamata ya watu wanaouza kazi za muziki zisizohalali. Hili ni jambo la kupongezwa ambalo lingeigwa na wasambazaji wote tatizo la wizi wa kazi za sanaa lingepungua sana. Kuna kitendawili cha muda mrefu kwanini wasambazaji wakubwa hawalalamikii wizi wa kazi za sanaa? Tusome habari hii nzuri iliyotolewa na mhariri wa Tanzania Daima kuhusu kazi hii nzuri ya Msama

VITA VYA PANZI FURAHA YA KUNGURU

$
0
0
Tunaibiwa hatuimbiwi. Hicho ni kichwa cha habari nilichokiona karibuni katika gazeti moja yakiwa ni malumbano kati ya wasanii kadhaa wa filamu kwa upande mmoja na Shirikisho la Filamu Tanzania, kwa upande mwingine. Katika historia ya biashara ya sanaa katika nchi hii, si mara ya kwanza hali kama hii inatokea. Wakati biashara ya kuanza kuuza kanda za muziki wa bendi za Tanzania inaanza, kulikuweko makundi yenye msimamo wa aina hii , walikuweko wasanii ambao walikuwa upande wa wasambazaji wa kazi za muziki wakiwatetea wasambazaji kuwa ni wakombozi wa tasnia. Wakati huo album ilikuwa ikiuzwa shilingi 30,000. Kulikuweko na wanamuziki ambao walikuwa kama wakala wa wasambazaji wakipita kwenye bendi na kuzishawishi kuuza kazi zao, hata baadhi ya viongozi wa CHAMUDATA walishiriki kuchukua kazi za wasanii na kuiuza album nyingi za bendi kwa mfumo huo. Uchunguzi mdogo utaonyesha kama kweli hawa walikuwa wakombozi au wezi.
Kulikuweko na kundi lililopinga mtindo huu wa kuuza kazi na hilo lilionekana kama kundi linalozuia maendeleo. Mfano mwingine ni RTD iliyokuwa na bado ni moja ya wauzaji wa kanda za wanamuziki, jitihada ya kuwasaidia wanamuziki wapate fungu lao katika biashara hiyo, ilipigwa vita na baadhi ya wanamuziki waliotetea RTD kuuza kanda hizo kwa maelezo kuwa RTD imesaidia sana wanamuziki. Mpaka leo kuanzia miaka ya tisini biashara hiyo inaendelea.
Picha iliyopo kwa sasa inafanana sana na picha ya wakati huo. Kuna wasanii ambao wanauhakika wa kuuza kazi zao kwa wasambazaji na pia wanauhakika wa misaada mingi ya kuwaweka katika hali nzuri mbele ya jicho la jamii hivyo wao wanatetea hali iliyoko kuwa hawaibiwi. Upande wa pili kuna wasanii ambao wamejikuta wanashindwa kusambaza kazi zao, wala kupata mahala pa kuuza kazi zao, labda pale wanapokubali kuuza kwa ujira mdogo ambao wanaona haukidhi hata malipo ya utayarishaji wa kazi, hawa wanalalamika kuwa wanaibiwa.
Simon Mwakifwamba Rais TAFF
Katika tasnia ya filamu kuna wadau wa aina tofauti, kuna wasanii waigizaji, kuna watengeza filamu, kuna wasambazaji, baadae kuna vyombo vya urushaji wa matangazo ya filamu na video kama vile TV, DSTV na kampuni kadhaa za usambazaji kazi kwa njia ya Cable, pia wahusika wengine wengi kama watunzi wa hadithi , waandishi wa script, waongozaji wa filamu na kadhalika. Kati yao hawa kuna  aina mbalimbali za haki. Wasanii waigizaji hulindwa na sehemu ya hakimiliki inaiyotajwa kama hakishiriki, na hawa kwa kawaida hulipwa moja kwa moja kutokana na nafasi walizoigiza katika filamu au umaarufu wao na kadhalika. Hivyo msanii anaingia makubaliano ya kulipwa aidha kwa kila scene au kwa ujumla wa  filamu nzima(Project). Hivyo kwa mtizamo huu wa mwanzo wasanii waigizaji huwa hawana cha kuibiwa kwani wanakuwa wamekwishalipwa na watengenezaji wa filamu. Kundi la pili ni la watengezaji wa filamu ambao wao ndiyo huwa  wanajukumu la kuwalipa waongozaji, waandishi wa script, na wasanii waigizaji,na washiriki wengine katika filamu. Hawa hutegemea kupata fedha zao kutokana na malipo wanayopata kwa wasambazaji. Hapa ndipo ugomvi wa nimeibiwa sijaibiwa unapopata kelele zaidi. Watengeza filamu wanalalamika kuwa wanawekewa masharti ambayo yanadumaza tasnia ya filamu. Baadhi ya masharti ambayo yamekuwa yakilalamikiwa ni wasambazaji kulazimisha ushiriki wa wasanii ambao wasambazaji wanaona ‘wanauza’, au hata kulazimishwa kubadili hadithi. Nilikutana na kikundi cha sanaa Iringa ambacho kilipewa masharti ya kumhusisha msanii fulani maarufu ndipo filamu yao ingesambazwa na msambazaji maarufu. Tatizo jingine ni kulazimishwa kuingia katika mikataba ambapo filamu nzima hununuliwa na msambazaji. Mwenye filamu huwa na haki nyingi katika filamu, kurudufu, kusambaza, kutafsiri lugha, kubadili kazi(kwa mafano kutumia kipande katika matangazo), kurusha katika vyombo vya habari, kupeleka nje ya nchi nakala za kazi husika, kuingiza nchini nakala za kazi husika, na kadhalika, sasa katika kuuza haki zote hizo hukabidhiwa anaenunua, jambo ambalo linaleta utata kwani msambazaji kazi yake ni kusambaza tu. Kubwa zaidi sheria ya Hakimiliki ya nchi yetu inaeleza kuwa hakimiliki hudumu kwa maisha yote ya mwenye hakimiliki, na miaka hamsini baada ya kifo chake. Sasa swali ni bei gani unaweza ukanunua haki zenye thamani ya umri huu? Katika nchi zenye mfumo bora wa utawala wa kazi za sanaa, msambazaji huingia makubaliano ya usambazaji kwa makubaliano yanayompa muda kamili wa usambazaji, eneo ambalo msambazaji anaruhusiwa kusambaza. Hii inampa mwenye kazi uwezo wa kubadili msambazaji pale anapoona kazi yake haisambazwi vizuri au haisambazwi kabisa. Katika nchi hii kutokana na wasambazaji kuhodhi kazi ya usambazaji utakuta kazi zinachelewa kusambazwa na hivyo kwa wahusika kukosa mapato au la filamu yao kutoka wakati usiomwafaka na hivyo kukosa soko na kubakia kubeba kawama kuwa hawakuwa na kazi bora. Watayarishaji hujikuta filamu zao zikionyeshwa kwenye TV, au katika vyombo vingine vya kurusha matangazo bila ya wao kufaid kitu, kwani wameshauza kazi hizo. Mfanya kazi moja wa TV hapa nchini aliniambia filamu wanaletewa na wasambazaji, msambazaji haki yake ni kusambaza biashara ya kurusha matangazo huwa si yake kamwe.
Jambo baya ambalo limeingia katika tasnia hii ya filamu ni juhudi za makusudi za kuwamaliza wasambazaji wadogo. Duniani kote kuna wasambazaji wakubwa na wadogo. Mfano una mtaji wa kuweza kusambaza filamu yako, hilo ni jambo zuri , kilichofanyika katika miaka ya karibuni ni wasambazaji wakubwa kushasha bei ya ya jumla kutoka shilingi 3000 kwa nakala hadi chini ya shilingi 2000 kwa nakala hivyo kuwazuia wasambazaji wadogo kuweza kufanya kazi. Hii imelazimisha kila mtengenezaji kuwasujudia wasambaji wakubwa tu ambao ndio hutoa masharti, na kudai kuwa hawajamlazimisha mtu kuja kwao.
Taratibu ambazo zinachukuliwa na wasanii wanodai hawaibiwi ni kumwendea msambazaji na kumtajia kiasi cha fedha ambacho kitahitajika katika kutengeza filamu na hupewa kiasi hicho kadri ya makadirio yao, na filamu hiyo huwa mali ya msambazaji. Kuna taarifa za wasanii wa aina hii kuwa na mikataba ambayo hairuhusu kutengeza filamu nje ya kampuni za usambazaji, aidha wengine kupewa malipo ya gari moja kwa kutengeneza filamu hata zaidi ya tatu. Ni wazi hapa ukosefu wa uelewa wa ukubwa wa biashara hii ndio unaoleta msanii kukubali malipo duni namna hii na kuona hajaibiwa.
Jambo lililowazi ni wasanii kuchukua muda na kupata elimu kuhusu haki zao ambazo wakizielewa zitawasaidia kuishi vizuri hata pale ambapo majina yao si maarufu tena , au wasambazaji watakapoamua kuwatosa kwa jili ya kuingiza damu mpya katika biashara zao. Hakuna kitu kinachodumu milele.
Swala la Serikali ya Tanzania kutokuelewa ukubwa wa biashara hii ni tatizo kubwa sana. Katika nchi nyingine serikali huwa na mkono katika shughuli za aina hii kwani ni chanzo kikubwa sana cha pato la taifa na nafasi yenye ajira nyingi kwa wananchi

Ugomvi unaoendelea sasa katika tasnia ya filamu unatimiza usemi maarufu wa wahenga- VITA VYA  PANZI FURAHA YA KUNGURU

Wanamuziki wawili wafiwa na baba zao wiki hii

$
0
0
Tom Nhigula

Karola Kinasha
Mwanamuziki Carola Kinasha na Tom Nhigula wamefiwa na baba zao katika wiki hii. Mzee Nhighula amezikwa makaburi ya Kinondoni, wakati Mzee Kinasha atazikwa baadae wiki hii Longido. Mungu awalaze wazazi wetu hao mahala pema peponi Amen

SI BUSARA KUUZA MASTER KWA MSAMBAZAJI

$
0
0


Mara nyingi utasikia msanii kauza kazi yake kwa msambazaji, hili hunishangaza sana. Sababu za kushangaa ni nyingi, ya kwanza kubwa ni kuwa msambazaji kazi yake kusambaza, sasa kwa nini umuuzie? Wewe ingia nae mkataba wa kusambaza kazi yako kwisha.
Kazi za muziki na filamu zina haki kama kumi hivi ambazo zimetajwa katika kifungu na 9(1) cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ya 1999 nazo ni;
i.               Kurudufu kazi
ii.              Kusambaza kazi
iii.            Kukodisha
iv.            Kuonyesha hadharani
v.             Kutafsiri
vi.            Kubadili matumizi ya kazi
vii.          Kufanya maonyesho ya hadhara
viii.         Kutangaza kazi katika vyombo vya utangazaji
ix.            Kutangaza kwa njia nyingine zozote
Wasanii wakiwa na Waziri Mkuu katika viwanja vya Bunge
x.             Kuingiza kazi nchini
Kwa hiyo utaona msambazaji kimsingi anahitaji zile haki mbili za mwanzo tu, hizi haki nyingine zinakuruhusu mwenye mali uendelee kufaidi matunda ya kazi zako. Ukiuza ina maana umeuza na haki nyingine nane ambazo anaweza asizitumie kamwe.
Sheria ya Hakimiliki ya nchi yetu inasema Hakimiliki hudumu kwa mwenye haki kwa maisha yake yote na miaka hamsini baada ya kifo chake. Wengi tunaona kazi nyingi tu ambazo zinaendelea kuwa maarufu miaka mingi baada ya wenye kazi kufariki, hivyo kuweza kunufaisha warithi wa mtunzi, sasa ukiuza kazi warithi wako umewaachia sifa tu kuwa uliwahi kuwa na kazi.
SI BUSARA KUKUBALI MKATABA WA KUUZA KAZI KWA MSAMBAZAJI

Shamba la bibi

$
0
0

Hebu jaribu kupata picha, umelima shamba lamba lako na kupanda mahindi ambayo umeyatunza vizuri na yako tayari kuvuna….. unaamka siku moja na kukuta kuna mtu kayavuna na ameanzisha biashara anapata fedha nzuri wewe huna hata fedha ya kula.
Au umenunua suti nzuri akaja mtu akaivaa harusini, kesho yake anakuja kukutaarifu jinsi walivyomsifia harusini kwa kupendeza na suti yako.
Hiyo ndio picha ilivyo katika shughuli za sanaa Tanzania. Na haswa katika mambo ya muziki na filamu.
Wasanii hufanya kazi ngumu ya kutunga na kufanya mazoezi kisha kurekodi kazi zao, kabla hawajafaidi kazi zao hukuta shamba lao likiwa linavunwa kwa njia mbalimbali. Wengine hurudufu kazi zao, wengine huzitumia kutangaza biashara zao. Wengine huzitumia kuhamasisha mikutano yao, wengine huziuza kwa kuwarekodia watu katika simu, katika yote haya mwenye shamba haoni mafao yoyote.
Kutokana na matumizi mengi ambayo yanaweza kutokana na kazi zilizotungwa, na kutokana na ugumu wa kudhibiti kazi hizi sheria zinazitwa za Hakimiliki hutumika katika kulinda maslahi ya mtunzi kwa upande mmoja na mtumiaji kwa upande mwingine.
Ulinzi wa hakimiliki umekuwa mgumu sana hapa nchini kwetu hasa kutokana na kuweko kwa utamaduni wa kutokuheshimu ubunifu wala sheria zinazolinda haki za ubunifu. Labda nitoe mfano, leo ukianzisha kibanda cha chips chenye mapambo tofauti na vingine, muda mfupi baadae mtaa mzima utajaa vibanda vinavyofanana na chako. Watu hawaoni shida kunakili ubunifu. Fundi seremala akibuni staili fulani ya makochi baada ya muda mfupi maseremala kila mahali wataiga staili hiyo ya makochi bila hata kuwaza kuwa wanaiba ubunifu.
Katika maeneo yote ya karibu ya vyuo na sehemu za elimu ya juu utakuta biashara kubwa ya mashine za fotokopi, kazi ya mashine hizi ni kurudufu maandiko na vitabu mbalimbali vya watu bila kujali kuwa waliotunga vitabu hivyo wanahitaji viuzwe ili wapate mafao yao.
Kwa masaa ishirini na nne kila siku redio na baadhi ya Tv hurusha hewani nyimbo za watu, tena kwa vipindi ambavyo hutangazwa wazi kuwa vimedhaminiwa na kampuni kubwa mbalimbali zenye kuheshimika. Vituo hivi vinamilikiwa na kuendeshwa na watu wanaoheshimika katika jamii kwa kuhamasisha vijana wajiajiri, lakini ikishafika kwenye eneo la kulipia matumizi ya kazi za wasanii kigugumizi kikubwa kinatokea.
Watetezi wa haki mbalimbali za wananchi wa Tanzania, watatetea kila haki lakini wakati wa kampeni zao watatumia kazi za wasanii na kuwa wagumu kulipia matumizi hayo. Wanasiasa wakiwa katika kampeni za kuwaeleza wananchi ni jinsi gani wakipata madaraka watatetea haki zao hutumia kazi nyingi za sanaa bila kuzilipia na wala hawaoni kuwa tayari kuna wananchi wanawanyanyasa kwa kutumia kazi zao bila kulipia.
Sheria za hakimiliki humpa mtunzi haki zifuatazo katika tungo zake;
(a)Kurudufu kazi
(b)Kusambaza kazi
(c)Kukodisha kazi
(d)Kutafsiri kazi
(e)Kubadili matum izi ya kazi
(f)Kuonyesha kazi hadharani-exhibition
(g)Kuifanya kazi hadharani-public performance
(h)Kutangaza kazi katika vyombo vya habari-broadcasting
(i)Kuwasilisha kazi kwa umma kwa njia yoyote
(j)Kuingiza kazi nchini
Mtunzi anaweza akaingia katika makubalianao na mtu mwingine ili kutumia moja au zaidi ya haki hizo ili kupata mafao yake.
Nadhani ukiangalia haki hizo hapo juu utaweza kuona jinsi haki za watunzi zinavyovyunjwa masaa ishirini na nne.
Ununuapo CD au DVD elewa kuwa umeipata kwa ajili ya matumizi yako binafsi, ukianza kuitumia kwa shughuli yoyote ile nyingine unaanza kuingilia haki zilizotajwa hapo juu. Hivyo basi kununua CD hakukupi haki ya kuanza kutoa nakala za CD hiyo, wala kuanza kuirusha redioni au kuipiga hadharani kwenye baa au hoteli, hapana, utahitaji kupata ruksa kuanza kutumia kwa kazi hizo za ziada.

Zijue Haki katika Hakimiliki

$
0
0

Hakimiliki ni haki zinazotolewa kwa mwenye hakimiliki. Haki hizi ziko katika mafungu mawili. Haki za kimaadili, hizi ni haki ambazo hazihamishiki umiliki wake, ni haki za kutambuliwa kama ndiye mbunifu au mtunzi wa asili wa kazi, au mshiriki katika kazi yenye hakimiliki.
 Haki nyingine ni Haki za Kiuchumi hizi ni haki ambazo huweza kuingiza kipato katika kazi ya ubunifu, na hapa hasa ndio ambapo kilio kikubwa kuhusu Hakimiliki kipo. Haki hizo ni zile zilizokwisha tajwa katika kifungu na 9(1) cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ya 1999 nazo ni;
i.               Kurudufu kazi
ii.              Kusambaza kazi
iii.            Kukodisha
iv.            Kuonyesha hadharani
v.             Kutafsiri
vi.            Kubadili matumizi ya kazi
vii.          Kufanya maonyesho ya hadhara
viii.         Kutangaza kazi katika vyombo vya utangazaji
ix.            Kutangaza kwa njia nyingine zozote
x.             Kuingiza kazi nchini

Matumizi ya majina katika Hakimiliki

$
0
0
Hakimiliki haitoi haki katika matumizi ya majina. Swala la majina linakuja katika tawi jingine la sheria za Milikibunifu linaloitwa Tradenames au majina ya biashara. Brela iliyoko chini ya Wizara ya Viwanda na Masoko ndiyo yenye mamlaka ya kusajili majina ya biashara, Hivyo ukiwa na jina na unataka kulisajili kisheria unaenda Brela nao hutoa ushauri kuhusu hilo. Lakini kuna majina ambayo ni ya kawaida na unapenda kusajili kama jina la biashara, hutaweza kusajili kama jina hilo tayari linatumika kwa biashara inayofanana na unayotaka kuanzisha. Kwa mfano unataka kuanzisha kampuni ya kutengeza tochi ukasajili jina la Malaika Torch Company, haitawezekana tena kwa mtu mwingine hapa Tanzania kuanzisha kampuni ya tochi akaiita Malaika, lakini jina hilo linaweza likasajiliwa na mtu anaetaka kutengeza mali isiyo na uhusiano kabisa na tochi. Mfano tuna jina Kilimanjaro, kampuni nyingi mbalimbali zimetumia jina hilo kama inavyoonekana hapo chini.





WARAKA WA KWANZA WA MAC TEMBA

$
0
0


Salaam nyingi kweni nyi wote wapenzi wa muziki hapa Bongo,leo kamanda wenu Mac Temba aka mwanaharakati wa Anti virus nataka kuwapa tafsiri na kuweka mambo sawa yote kuhusiana na mambo kibao yanayopindishwa na kuficha ukweli wa Vuguvugu la kudai haki sawa na uwanja huru wa kufanya sanaa hapa Bongo,kwa jina la mtaani limepewa jina la “Anti virus”

Anti virus ni mkusanyiko wa watu mbalimbali wenye taaluma mbalimbali na uwezo mbalimbali ambao tunaamini kuwa sanaa hii ya muziki inaweza kuwasaidia vijana wengi hapa bongo na pia kuisaidia nchi yetu kupata kodi ambayo itasaidia kuleta maendeleo na kuisogeza nchi yetu mbele kama wenzetu Afrika kusini,Nigeria.Kamwe huu si mgomvi na mtu mmoja wala chombo kimoja cha habari.

Kinachodaiwa hapa ni haki na usawa katika sanaa na malipo sahihi kama wanavyolipwa wakenya na wanaigeria wakija hapa kufanya maonyesho mafupi ya muda wa saaa moja na kuchota mamilioni mengi toka kwa makampuni ambayo yanapata faida toka kwa watanzania hawa ambao wasanii wao wa ndani wanaishi maisha mabovu sana na wala hawakumbukwi na makampuni haya ya bidhaa ambayo hupata mamilioni ya faida toka wa watanzania hawa.

Sanaa na soka ni fursa pekee ya kumfanya mtoto toka katika familia masikini kuweza kuwa milionea ama kufanikiwa kujinyanyua toka katika maisha mabovu mpaka maisha bora,ni kama mpira ulivyo katika nchi ya Brazil,soma historia za wanasoka kama wakina Ronaldo de Lima na wekina Pelle soka ndilo lililowafanya waweze kujiinua na kuweza kuzisaidia familia zao kupata mafanikio na kuishi maisha bora nay a kifahari.

Hakika naomba niweke sawa hapa Anti virus movement ya kudai haki si ugomvi kati ya Sugu na Ruge bali ni vuguvugu la wasanii wa zamani wanaamini kuwa game ya muziki haiendi sawa na kutaka mambo yawe wazi na BASATA na COSOTA kuundwa upya ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi na kupunguza haya malalamiko na pia watu hao wanaoitwa mapebari katika muziki(hao Virusi katika muziki wanaotafuna mamilioni ya wasanii wetu wachanga wakome),hii ndio sababu ya anti virus na hakika kadiri muda unavyozidi kwenda nashukuru watanzania wanazidi kutuelewa.
Sugu ndiye msanii pekee anayeweza kusimama mbele na kujiita Legendary katika muziki huu na si mwingine yeyote maana wengi wao ni kama “fisi maji” mnaotaka mabadiliko lakini hamtaki kuongea eti “mtanyimwa airtime redioni” acheni ujinga na kujifanya wanaharakati wakati mnaendelea kunyonywa na mnaishi maisha mabovu wakati sanaa yenu ni kubwa sana na ndiyo kazi pekee inayowafanya muishi mjini,maana wengi wenu mliacha shule kukimbilia katika sanaa cha kushangaza mnaogopa kusimama na kutetea haki zenu za msingi.

Mapambano dhidi ya vuguvugu la kupinga unyonyaji huu hayajaanza jana wala juzi,Solo Thang mwana hiphop anayeishi na kufanya kazi Ireland aliwahi kuingia katika beef na redio moja hapa kwa kudai haki na kuwachana kuwa wanaiba haki za wasanii,wakampiga vita na kumtengenezea kila hila ili kumpoteza,hata wasanii ukiongea nao wanajua haya ila eti wanamuogopa huyo virus eti atawapoteza na kuwanyima airtime ila wako tayari kuendelea kusafriki mikoa yote kwa show ya laki 4 wakati wanaingiza mamilioni ya shilingi.

Inashangaza eti msanii kama Lina eti anaambiwa ana mafanikio kwa kuweza kununua gari aina ya “Vitz” baada ya kuuza albamu na kufanya show kibao,je haya ni mafinikio kweli kwa mauzo ya albamu Bongo?haya ndio mambo tunayopigia makelele maana zamani adui wa wasanii alikuwa mdosi lakini siku hizi mpaka huyo Virus sasa ndiye anayeamua kusambaza albamu za wasanii wetu na nani apewe shilingi ngapi kwa albamu yake.

Ni wasanii wangapi wa hapa kwetu wenye kuishi maisha ya kueleweka na kumiliki vitega uchumi na kuweza kuendesha maisha yao???hakika hawazidi kumi kwasababu wengi wanapambwa redioni lakini ki uhalisia hawana cha maana,hebu ona wsanii kama Mr Nice,Bushoke,Gangwe Mobb,Feroos,East Coast Team walivyotumiwa na alivyotupwa na hao wadau,Sio kwamba wametumia pesa vibaya bali asilimia kubwa ya pesa hizo huliwa na hao wadau na kuahidiwa eti promotion ya albamu ijayo.

Hili si sawa ndio maana katika hili tunataka wanaojibu hoja za Anti virus wajibu hoja na sio propaganda za kitoto maana watu wameamka na wanataka majibu na uwanja huru katika sanaa,kila mwenye fursa na uwezo katika sanaa afanye bila kubughuziwa,sanaa iwe huru na vyombo vinavyosimamia sanaa viweze kufanya kazi bila mikono ya hawa virus aka mabepari wa sanaa wanaopigwa vita.Huu sio ugomvi wa watu wawili hapana,haya ni mapambano ya kudai haki na usawa katika sanaa yetu maana sanaa si ya watu wachache.

Kama mambo haya ya sanaa yetu yangeweza kuwa wazi na fair tungeweza kuwa na wasanii wenye mafanikio kama lady Jaydee wengi sana na hakika wangeweza kuwavutia mabinti wengi kuingia katika sanaa hii lakini ukimtoa lady jaydee taja mwanamuziki mwingine mwenye mafanikio kama yeye,Kuna siku moja niliona mahojiano na msanii mmoja mkubwa wa hip hop bongo anayejiita legendary akisema mafanikio yake katika gemu toka aanze miaka zaidi ya kumi nyuma ni nyumba na gari Spacio!!! Daah inasikitisha sana unapoona msanii kama Nonini wa juzi juzi sasa hivi ana mafikio makubwa na hafanyi show chini ya dola 2500 na ukiwataka P unit ni dola 3000 lakini katika show hiyohiyo msanii wa bongo analipwa laki 4 na wengine mpaka bure kwa ahadi ya kupewa airtime redioni kwao,huu ndio wizi tunaousema uishe maana ni lini msanii wetu atakuwa na mafanikio kama malipo ndio haya.

Hofu kubwa ya kundi hilo la mafisadi wa sanaa hapa Bongo ni kuwa haya mambo yakiwa wazi watakosa pa kuiba na kufisadi ndio maana wanapandikiza mamluki na kujibu majibu ya ki propaganda na kukimbia hoja za msingi,jambo moja ambalo wanapaswa kulijua ni kuwa hakuna jambo ambalo halina ncha.

katika hili muda umefika,jana kwenye facebook mambo mengi yamejiri na comments kibao mmoja wa wadau wa muziki Pkay alindika “the fall of Roma empire…wake up kids…maji yakizuiwa njia hutafuta mkondo mwingine,someni alama za nyakati”

Dada Maria Sarungi- Tsehai yeye aliubatiza huu mwamko kama Sugu phenomenon katika ukurasa wake wa facebook jana na kusema “Angry young men ambao wamechoka na wameamua kujiexpress kupitia muziki,ni hatua nzuri ila isiishie hapo…”

Carren Flora Mgonja kwenye wall yake ameeandika”Asanteni vinega kwa kutupa show tukioikosa kwa long tyme,I salute my brothers,safi sana Adili na songi lako peke yangu,Soggy na kibanda cha simu”

Hili mimi nililijua litafika hapa maana hakika ni jambo ambalo tulikiwa tunalizungumzia mara kwa mara katika mijadala na wadau wa muziki huu kuwa kuna watu wachache wanaohodhi mamlaka na kufanya mambo katika sanaa yasisogee mbele kwa manufaa yao binafsi,napinga sana suala hili “eti muziki wetu haulipi”nani kasema muziki haulipi?mbona hao wadau ni muziki huu huu umewafanya mpaka wameweza kufungua TV,muziki huu huu ndio unaowafanya wao kununua magari ya kifahari.

Nguvu ya mabadiliko ya watu haipingwi kwa vijembe redioni wala maneno ya shombo,bali kwa Hoja zenye msingi na zenye majibu na si kwa hoja nyepesi jamani,wasanii wengi wamejazwa fikra kuwa huu ni ugomvi binafsi kati ya watu wawili,hakika sio kweli,suala la Malaria No more limepita sasa tunasonga mbele na kutaka kila msanii kweli apate kipande chake halali na kuacha kutengenezewa wasanii na kikundi kimoja cha watu kwa maslahi yao.Miaka miwili iliyopita walianzisha mizengwe eti Hip Hop hailipi na kuwavuruga sana wasanii na wale wachache wasioweza kupambana wakaamua kuanza kubana pua ili wapewe airtime.

Kwa muda mrefu nimekuwa mdau na naufahamu muziki huu kwa upeo mkubwa sana na ndio maana nayaongea haya bila woga,ifike muda kila mtu akafanya jambo analolijua na sio kubahatisha,kuna jamaa mmoja eti ni “music director “wa redio moja hivi ya fm hapa mjini eti yeye kazi yake ni kusikiliza nyimbo na kutoa kasoro na marekebisho cha kushangaza huyo anayeitwa music director hana hata diploma ya muziki huo,unawezaje kukosoa kitu amabcho hukijui na kutenda haki???haya ndio mambo ya kimagumashi yanayoharibu muziki wetu,get a life boy na kama unataka kufanya mambo nenda shule japo diploma itakupa msingi wa kufanya hayo.

Miaka michache iliyopita alivuma msanii Mb Doggy na kutajwa kuwa ameuza kopi zaidi ya laki moja katika siku mbili za mauzo ya albamu yake ya “Lafifa”daah akapewa coverage kubwa na mengi yakasemwa ooh kavunja rekodi mpaka kawafunika jamaa wa bendi lakini hebu mtafute Mb Doggy leo kaa nae umuulize uhalisia wa yaliyotokea,utasikitika na kuduwaa,leo hii Mb Doggy anapambana kurudi upya kwenye game japo apate hela ya kuishi,hii ni hatari sana.

Wasanii wa bongo amkeni acheni kufanywa misukule na kutumiwa kama daraja la kupata mafanikio ya watu wachache na aminini kuwa hata nyie mnauwezo wa kufanya makubwa na kumiliki magari ya kifahari kama chameleon,Nonini,Bebe Cool ama Nameless na kuacha kuishi maisha ya kuunga unga wakati you got all the means to be on Top,Bila kuamka na kupigania hili hakika mtazeeka na kukosa la kuwaelezea watoto na wajukuu,Hata marehemu mzee Kipara wa kaole alikuwa kijana kama nyie hebu ona maisha ambayo alikuwa anaishi mpaka mauti ikamfikia.inasikitisha na bila kutumia ujana wenu sahihi hakika mtakuwa mizigo huko uzeeni.

Waraka wa pili utakujia tena jumatatu ijayo>>>>hii ni kwa ajili ya wapenda muziki wote na kupata ufahamu ya kinachoendelea kwenye Anti Virus Movement ya kuokoa muziki huu wa Bongo usiendelee kupotea na kufaidisha kundi dogo la mabepari aka Virusi.

ALUTA CONTINUA….
Anti Virus Activist MAC

Jifunze Hakimiliki na Hakishiriki

$
0
0

 Nawaletea mfululizo wa makala za mafunzo ya Hakimiliki na Hakishiriki. Waandishi mnaruhusiwa kunukuu makala hizi ili ziweze kusambaa kwa wingi kadri iwezekanavyo
1) Nini madhumuni ya ulinzi wa Hakimiliki?

Hakimiliki hulinda kazi za kimaandishi na kazi za sanaa kwa kutoa haki mbalimbali kwa watunzi wa kazi hizo. Hakimiliki hailindi wazo bali hulinda matokeo ya wazo. Matumizi ya wazo kutokana na Hakimiliki hayalindwi katika Hakimiliki, kwa mfano mtu akiandika makala juu ya jinsi ya kutengeneza aina mpya ya boti, mtu mwingine akaweza kutengeneza boti kwa kutumia maelekezo yale atakuwa hajavunja sheria ya Hakimiliki. Ili itakuwa ni makosa mtu kutengeneza nakala za maandiko hayo na kuyauza bila ruksa ya mtunzi. Ili kazi ilindwe ni lazime iwe katika hali ya kushikika bila kujali madhumuni au ubora wa kazi yenyewe. Hivyo basi ukiandika shahiri si lazima lichapwe kwa mashine hata kama ukiandika kwa kalamu kwa muandiko mbovu, shahiri hilo litalindwa na hakimiliki.


2) Hakimiliki hutoa ulinzi wa aina gani?

Hakimiliki kwa kawaida hutoa ulinzi wa haki za aina mbili, ambazo hujulikana kama Haki za Kiuchumi (Economic Rights), na Haki za Kimaadili (Moral Rights).
Haki za Kiuchumi ni zile haki ambazo zinamuwezesha mwenye Hakimiliki kufaidi mapato kutokana na kazi zake. Hivyo basi mwenye Hakimiliki anakuwa na mamlaka ya kuruhusu watu wengine watumie kazi zake ili aweze kupata pato kutokana na kazi hizo. Hivyo mwenye hakimiliki ataweza kuruhusu kazi zake kurudufiwa au kama ni mchezo kuonyeshwa hadharani, kama ni wimbo kupigwa redioni, na kwenye vyombo vingine vya utangazaji na pia katika mtandao wa intaneti.
Haki za kimaadili zinamuwezesha mwenye hakimiliki kutambulika katika kazi yake. Kwa mfano kama ni kitabu kuweza kutajwa kuwa ndie mtunzi wa kitabu kile, au ni muziki muhusika kutajwa nafasi yake katika wimbo husiki. Je ni mtunzi, mwimbaji, producer na halikadhalika Pia haki hizi humuwezesha mwenye kazi kuzuia kutolewa hadharani kwa kazi yake, na kuzuia matumizi ya kazi yake ambayo ataona yatamdhalilisha au kuharibu maana ya kazi yake.
.

Mheshimiwa Waziri Dr E Nchimbi, Serikali haina nia thabiti kumaliza wizi wa kazi za sanaa

$
0
0

Kwa  Mheshimiwa
Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo.

WIZI WA KAZI ZA SANAA.
Mheshimiwa  nategemea usalama na unaendelea vizuri na kazi. Mimi si mgeni kwako, nimeshafika ofisini kwako tukaongea mengi  sana kuhusu sanaa na hasa wizi wa kazi za sanaa. Ilikuwa ni mapema baada ya wewe kuteuliwa tu kuwa Waziri wa Wizara yetu. Nilitoka ofisini kwako nikiwa na furaha na matumaini, lakini naona muda unakwenda maumivu yako palepale.  Nimesikia tena si mara moja hata Mheshimiwa Rais ‘akilaani’ wizi wa kazi za sanaa, lakini kila mara napata picha kuwa serikali haijaamua kumaliza tatizo hili. Mambo mengi yananihakikishia ukweli wa picha yangu hii.
Kwa kweli wengine tuliposikia kuwa safari hii wasanii tuko Wizara moja na Habari tukaelewa tatizo letu la kuibiwa na vyombo vya habari litaisha, miezi imepita na sasa miaka inaanza kuhesabika hakuna dalili zozote za kuonyesha mabadiliko ya unafuu wa wizi huo. Hebu tuanze na TBC, chombo ambacho kiko chini ya Serikali yenyewe.
 Kuanzia katikati ya miaka ya 90 wakati huo ikiwa RTD, taasisi hii ilianzisha biashara ya kuuza kanda za muziki unaojulikana kama zilipendwa, pia kulikuwa kunauzwa kanda za ngoma za  makabila mbalimbali, na pia kanda za vipindi maarufu kama vile Pwagu na Pwaguzi. Hili halikuwa tatizo , tatizo ni kuwa baada ya kupata fedha za mauzo hayo, TBC hawakushughulika kabisa kukumbuka kuwalipa wasanii ambao ndio walikuwa watunzi, waimbaji, na wapigaji wa vyombo, na waigizaji  mbalimbali vya kazi hizo, haihitaji busara kubwa kuona huu ulikuwa wizi wa wazi ukiendelezwa na chombo cha serikali, na kwa vile  risiti za serikali zilitolewa, serikali yetu wenyewe ilikuwa inafanya biashara ya Piracy au uharamia wa kazi za muziki. Aibu hii iliendelea hata baada ya kuanza kutekelezwa kwa sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki No7 ya 1999.
Risiti ya manunuzi ya CD

Ganda la nje la CD zitokazo TBC
Pamoja na waraka huu  naambatanisha picha ya ganda la CD lililotengenezwa bila hata kujali thamani ya kazi zilizomo katika CD hiyo ambayo ina nyimbo za bendi niliyoshiriki kuwemo. Pia naambatanisha nakala ya risiti ya manunuzi ya CD hiyo.
Aibu iliyoje chombo cha serikali kinavunja sheria zilizotungwa na serikali yenyewe. Si hivyo tu, kuanzia mwaka 2003 Regulations kuhusu malipo kwa ajili ya matumizi ya kazi za muziki zimekuwa tayari, ungelitegemea kuwa TBC Radio na TV zingekuwa mstari wa mbele kutekeleza sheria na kuanza kulipa kwa ajili ya matumizi ya kazi za muziki, lakini mpaka leo dhuluma hiyo inaendelezwa na chombo hicho kwa kutumia kazi za wasanii kwa masaa 24 bila kulipa senti tano. Naongelea kwanza TBC kwa kuwa ni Taasisi iliyo chini ya serikali na ilipaswa kuwa ya kwanza kufuata sheria. Usugu huu wa serikali yenyewe kuendelea kuwaibia wasanii ndio unaovipa vichwa hata vyombo vingine vya utangazaji viendelee kugoma kuwalipa wasanii kwa kisingizio kuwa vyombo hivyo vinawa’promoti’ wasanii.
Mheshimiwa tunajua hili liko katika uwezo wako na tunaimani utalitatua bila wasanii kufikia  kulazimika kuonyesha hisia za kuchukia kwao.
Swala la wizi wa kazi za sanaa linalindwa na sheria ambayo iko chini ya Wizara ya  Viwanda na Biashara Viwanda na Masoko, hili ni tatizo hivyo kuna umuhimu wa kutafuta njia ya kuwa na kamati ya pamoja ya Wizara mbili hizi. Kuna mengi ya ajabu yamekuwa yanaendelea katika kukwamisha kutekeleza kikamilifu sheria hii. Naomba nitoe mifano, mwaka 2001 ilitengenezwa kamati iliyoitwa National Anti Piracy Committee, mimi ndiye niliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati hii. Kamati hii ilitakiwa kutengeza Regulations za kuwezesha kutekelezwa kwa sheria ya Hakimiliki hasa kipengele kilichotaja kuwa ‘kazi zote za muziki na filamu zitatakiwa ziwe na alama ya kuzuia uharamia wa kazi hizo yaani anti piracy device’.
Kazi hii ilifanyika kwa taabu sana kwa mara nyingi kukosa ushirikiano na Taasisi nyingine za serikali ambazo zilikuwa ni wajumbe katika kamati hii, wajumbe walitoka BASATA, COSOTA, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Forodha, Vyama vya Muziki,wafanyabiashara wasambazaji wa kazi za sanaa, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Elimu na Utamaduni na kadhalika. Hatimae kazi hii ilimalikamilika na Regulation hizo kuwa tayari. Regulations zikielekeza kuwa kazi zote halali za muziki na video zilitakiwa kuwa na stempu au sticker kwa mfano wa ile iliyoko katika vinywaji vikali au sigara, japo hii ilikuwa na masharti tofauti kidogo na hizo stempu au sticker zilizotajwa, na hata jina ikapewa ikaitwa HAKIGRAM. Regulation hii ilitakiwa kutiwa saini na Waziri wa Viwanda na Biashara wakati huo ili ianze kazi, Waziri husika kwa wakati huu akiwa Mheshimiwa Ngasongwa. Mheshimiwa Waziri alifanya kazi yake na  alitia saini regulation hiyo ili iweze kutangazwa katika gazeti la serikali na kuanza kufanya kazi, cha ajabu nakala zote zilizotiwa sahihi zilipotea hapo hapo Wizarani!!!!!!!!. Baada ya Uchaguzi 2005 Mheshimiwa Waziri Karamagi alilazimika kutia saini nakala nyingine, na ndipo kilipoanza kizungumkuti cha serikali kutokutoa fedha za kuwezesha kuanza kununua sticker za kwanza za kuwezesha kutekeleza zoezi hilo. Na mpaka leo zoezi hilo halijafanyika. Kama nilivyosema kuna mengi ya ajabu yanayoendelea katika swala la ulinzi wa kazi za sanaa. Miaka miwili iliyopita zikaweko habari kuwa swala hili la kumaliza tatizo la wizi wa kazi za sanaa limeanza tena kushughulikiwa na Ikulu. Kwa mshangao afisa moja aliyejitambulisha kuwa anatoka TRA aliniomba nimueleze matatizo katika tasnia ya muziki kwani katumwa na Ikulu ashughulikie matatizo hayo na kuweza kuanzisha sticker kwenye kila kazi ya sanaa, na kuwa yeye ni mtaalamu sana hata Nigeria walimuita yeye akawasaidia!!!!!nilishangaa kwani hilo jambo lilikwisha tengenezewa hata Regulation ila kutekelezwa kwake ndio kilikuwa kumekwama hivyo sikuelewa kwanini jambo ambalo lingekamilika kwa kupiga simu COSOTA  na kupata maelezo na kuanza kutekeleza. Pia  hatukuweza kuelewana na Mheshimiwa yule kwa kuwa kwanza alikuwa amekuja sehemu niliyokuwa napiga muziki na ilikuwa ni zaidi ya saa 6 usiku, na pili alikuwa amelewa kwa hiyo ilikuwa ni kazi bure kuelewana nae, nilimwomba anitafute wakati akiwa mzima sijamwona mpaka leo.
COSOTA ndicho chombo ambacho kinashughulikia mambo ya Hakimiliki kwa mujibu wa sheria ya nchi yetu. Katika Bodi iliyoisha muda wake 2006, ambapo pia nilikuwa mjumbe tuliona kuna haja ya kufanya marekebisho mengi katika chombo hiki, ikiwemo kurekibisha sehemu mbalimbali za  sheria iliyopo ya Hakimiliki, ili kuwezesha kuweko na ulinzi unaofaa wa haki za wasanii. Jambo hili lilianza kutekelezwa. Katika mkutano mkuu wa COSOTA wa mwaka 2007 ambao ulikuwa ni Mkutano Mkuu wa mwisho kwani haujafanyika mwingine tena, ilichaguliwa Bodi mpya, bodi hii hupitishwa na Waziri wa Viwanda na Biashara baada ya yeye kuteua Mwenyekiti wa Bodi. Jambo la kushangaza miezi kadhaa ilipita hadi kufikia Bunge la Bajeti la mwaka 2008, Mheshimiwa Waziri alikuwa hajapitisha Bodi hiyo, pamoja na kuulizwa swali hilo wakati wa kutoa makadirio ya Bajeti ya WIzara yake Mheshimiwa Waziri alijibu kuwa jambo hilo liko mezani kwake, ushahidi wa Hansard utaonyesha hilo. Hata lilipofika Bunge la Bajeti la mwaka unaofuata 2009, bado Mheshimiwa Waziri alikuwa hajakamilisha kazi hii na aliulizwa tena na Mheshimiwa Martha Mlata(MB), ambaye ndiye aliyekuwa kamuuliza 2008, akajibu kuwa hilo amekwisha lishughulikia, lakini kwa mshangao majina ya wajumbe Bodi yaliyopitishwa si yale ambayo wanachama walichagua kwenye Mkutano Mkuu wa 2007, bali lilikuwa chaguo la Mheshimiwa Waziri.
Huu ni mwaka 2011 mwishoni karibu miaka mitano COSOTA haina Board, Je, ilikuwa inapataje ruzuku? Audited reports zilikuwa zinapitishwa na nani?
COSOTA hukusanya fedha kwa niaba ya  wasanii bila Bodi iliyoteuliwa na wasanii kutakuwepo vipi ushahidi kuwa fedha zao zinatumika kadri ya mujibu wa Katiba ya COSOTA. Mipango yote iliyokuwa imeanzishwa na Bodi iliyopita imepotelea wapi? Mheshimiwa narudia tena kuna mambo ya ajabu sana katika utekelezaji wa Serikali katika kulinda haki za wasanii wa nchi hii.
Utafiti uliofanywa karibuni(2009) unaonyesha katika tasnia ya MUZIKI peke yake mapato kutokana kazi hizi ni Tshs Bilioni 78. Pia ikaonyesha ni asilimia 12 tu ya wanaopata fedha hizi wanaolipa kodi. Serikali ingepata kiasi cha Bilioni 18 kutokana na kodi. Mheshimiwa ukikumbuka kuwa Bajeti ya Wizara yako haifiki hata Bilioni 7, nadhani unaweza kupata picha ya ukubwa wa ukwepaji wa kodi, na hapa hakujaguswa sekta inayokuja juu sana ya filamu. Kuanza kufanya kazi zile sticker kungewezesha serikali kupata takwimu ambazo zingewezesha kukusanya kodi stahili. Pia wasanii wangeweza kupata stahili yao ya malipo kutokana na kazi zao.  Tumeona viongozi wakuu mkishiriki katika uzinduzi wa album mbalimbali za wasanii, je mnajua kuwa mnaemfanyia promotion si msanii ila msambazaji wa kazi ambaye kama tunavyoona hata kodi halipi?
Mheshimiwa kwa kuwa wasanii tuko chini ya Wizara yako tafadhali sema neno moja tu mambo yabadilike. Pia tunaomba  nyinyi Viongozi wa juu kabla hamjatoa matamko kuhusu wizi wa kazi za sanaa tungewaomba mpate taarifa kamilifu kuhusu sekta hii. Kutegemea kupata taarifa sahihi kutoka kwa mfanya biashara anaefaidi mapato kutoka kwa kazi za wasanii na kutegemea atakuwa kweli ni jambo ambalo linashangaza sana
Ni mimi mwanamuziki

John Kitime

Jifunze Hakimiliki na Hakishiriki (II)

$
0
0

3) Hakimiliki inapatikana vipi?



Hakimiliki hupatikana na kuanza kulindwa mara kazi inapokuwa katika hali ya kuweza kushikika bila kuweko na taratibu zozote za usajili. Kwa njia hii kutambulika kwa Hakimiliki kuko tofauti na haki nyingine katika Milikibunifu kama vile Hataza, au Majina ama alama za biashara ambapo ni lazima kusajili kazi. Taratibu hizi za kutoa haki moja kwa moja katika Hakimiliki ni kutokana na makubaliano yaliyomo katika Berne Conventions.

Mwaka 1952 alama ya © ilitambulishwa na UNESCO kama ndio kitambulisho cha kazi inayolindwa na Hakimiliki. Japo kuwa kama ilivyotajwa hapo juu si lazima kusajili kazi ili ilindwe, sheria za nchi mbalimbali huweka taratibu za kusajili kwa hiyari (voluntary registration). Kwa hapa Tanzania COSOTA ndio imepewa jukumu la kusajili kazi za hakimiliki. Hii zaidi husaidia katika ushahidi wa nani mwenye mali kama italazimika kufanya hivyo.



4) Hakimiliki ni mali ya nani?

Kimsingi, mwenye hakimiliki ni yule aliyebuni kazi Fulani kwa mara ya kwanza. Mara nyingi hujulikana kama mtunzi au mbunifu. Ikiwa watu wengi walishirikiana katika kutunga kazi hiyo kwa lugha ya Kiingereza hujulikana kama joint authors. Lakini ikiwa watunzi ni waajiriwa, na wametunga kazi hiyo katika shughuli zao za kazi sheria ya nchi yetu inasema mali ni ya muajiri, labda pale ambapo pana mkataba unaoeleza hali tofauti na hiyo. Katika nchi nyingine mwajiri lazima apate ruksa ya kimaandishi kutoka kwa mtunzi ili kutumia kazi zilizotungwa.



5) Mwenye Hakimiliki anafaidi vipi haki zake?

Hakimiliki humpa mwenye hakimiliki haki zote katika matumizi ya kazi yake. Kimsingi mtu yoyote atakaetaka kurudufu au kuzitoa hadharani kazi zinazolindwa na hakimilikilazima aingie katika mkataba na mtunzi wa kazi. Mara nyingi watunzi hutumia ‘record companies’ au vituo vya utangazaji katika kutoa kazi zao hadharani. Mwenye hakimiliki anapewa mamlaka ya kuweza kutoa leseni ya matumizi ya kazi yake kwa makubaliano, japo kuna nchi nyingine huruhusu mtunzi kutoa ruksa (assign) haki zake zote kwa mtu mwingine kwa malipo ya mara moja (lumpsum) au kwa kupata asilimia fulani ya mapato ya kazi hiyo. Lakini lazima ikumbukwe kuwa kwa sheria ya nchi yetu, hakimiliki huwa ni ya mwajiri katika hali ambayo mtunzi anakuwa ameajiriwa, hivyo mtunzi ataaishiwa kupewa mshahara tu kutokana na kazi yake.

Jifunze Hakimiliki na Hakishiriki (III)

$
0
0

6) Je unaweza kutumia kazi yenye hakimiliki bila kupata ruhusa?



Hakimiliki huruhusu matumizi yasiyohitaji ruksa. Katika nchi yetu matumizi binafsi yanaruhusiwa bila kupata ruksa. Kwa mfano ukitaka kutengeneza nakala za CD au DVD kwa matumizi binafsi. Pia unaweza kutoa nakala kwa ajili ya kutumia kwa mafunzo lakini nakala hizo hulazimika kuharibiwa mara baada ya somo. Vitu vya maandishi kwa mfano sheria au vitabu vikubwa vya dini kama Biblia na Koran havina hakimiliki, kwa hiyo vinaweza kutumika bila kulazimika kupata ruhusa kutoka kwa mtu yoyote. Japo matokeo ya kazi hizo hupata hakimiliki. Kwa mfano  mtunzi akichukua aya ya Biblia na kutunga wimbo, wimbo huo hulindwa na sheria za Hakimiliki japo mashahiri yanauruhusiwa kutumika na mtu mwingine yoyote bila kulazimika kutafuta ruksa. Kutokana na kazi nyingi kuruhusiwa kunakiriwa kwa matumizi binafsi, kuna nchi zimeanzisha taratibu za ‘Blank Tape Levy’ ambapo kodi hutozwa kwa CD, DVD, na kanda zote tupu kwa kuelewa kuwa vifaa hivyo lazima vitatumika katika kunakiri kazi, japo zinaweza kuwa si za kufanyia biashara. Mapato ya Blank Tape Levy kuwa ni sehemu ya gawiyo kwa wanachama wa Collecting Society.



7) Hakimiliki huindwa kwa muda gani?



Mbunifu wa Tanzania hupewa ulinzi wa Hakimiliki kwa kipindi cha maisha yake yote na miaka 50 baada ya kifo chake. Katika Umoja wa Ulaya (European Union) ulinzi ni maisha yote na miaka 70 baada ya kifo cha mtunzi. Lakini ulinzi huu ni kwa Haki za Kiuchumi tu. Haki za kimaadili hazina ukomo, hii ina maana kwa mfano umetunga kitabu, hata kikibadilishwa wachapaji mtunzi utabaki ni wewe tu hata ipite miaka mia. William Shakespear alitunga vitabu kadhaa vikiwemo The Merchant of Venice na Julius Ceasar, Mwalimu Nyerere alitafsiri vitabu hivi, hivyo juu ya ganda la kitabu huandikwa mtunzi William Shakespear, kimetafsiriwa na Julius K Nyerere


Hakishiriki ni nini?

$
0
0


Hakishiriki ni haki wanazopewa wadau ambao si watunzi lakini ushiriki wao umewezesha kazi ya mtunzi kufika au kuonekana hadharani. Kati ya hao ni wale ambao wanaotengeza kusambaza na kuziweka hadharani kazi zitokanazo na ubunifu kwa mfano.-
 * Performers, mwanamuziki ukipiga wimbo ambao hukutunga unalindwa na hakishiriki
* Actor-unapoigiza scene ambayo hukutunga unalindwa na Hakishiriki
 * Producers of sound recordings-wale watayarishaji wa kazi zilizorekodiwa,
* Broadcasting Organisations- vyombo vya utangazaji, pale wanapotumia ubunifu kutunga aina ya vipindi, mara nyingi sana nimesikia watangazaji wakiwananga wanamuziki kwa kuiga muziki wakati wanatumia kipindi ambacho wao wenyewe wameiga toka chombo kingine cha utangazaji. 
Ulinzi wa haki hizi unafanana sana na ulinzi wa Hakimiliki, japo kwa mfano kwa sheria za nchi yetu ulinzi huu huwa wa miaka 20 kuanzia siku kazi imewekwa hadharani.

Zijue Performing na Mechanical Rights katika muziki

$
0
0

Ukitunga wimbo na ukiiweka katika hali ya kushikika mara hiyo unaanza kupata haki zote za wimbo huo. Wimbo ni mali itokananyo na ubunifu hivyo moja kwa moja unapata haki zinazostahili kutokana na mali hiyo na ni mali yako kama vile mali nyingine,gari, kuku, nyumba. Mara wimbo utakapokuwa tayari kutumika ni muhimu kusajili katika sehemu husika ili uweze kupata ulinzi na stahili zitakazopatikana kutokana na mali hiyo. Kuna haki za aina mbili, Performance Rights na Mechanical Rights.
Performance Rights ni zile haki zitokanazo na tungo ya muziki kutumika hadharani au kurushwa hewani. Hii inajumlisha pamoja na muziki kupigwa na Live Band na, au hata muziki uliokwisha rekodiwa kupigwa hadharani katika sehemu za hadhara kama restaurants, bar, klabu za usiku, kwenye maharusi, madisco na kadhalika. Performance rights pia ni haki zinazoambatisha muziki kurushwa hewani kupitia radio na televisheni. Kutokana na kuweko kwa haki hizi, watu binafsi na makampuni ambayo yangependa kutumia kazi hizo ni lazima wapate ruksa kwa mwenye mali na hivyo mwenye wimbo kupata royalties kila wimbo wake unaporushwa hewani au kutumika hadharani. Kutokana na kuwa si rahisi kukutana na kila mwenye wimbo vyama vya ukusanyaji mirabaha, collecting societies hufanya kazi ya kuruhusu matumizi na kasha kukusanya mirabaha kwa niaba ya watunzi. Hapa kwetu Tanzania COSOTA ndio chama kilichopewa dhamani hiyo.
Mechanical Rights ni zile haki zinazohusiana na kuweka tungo katika vinasa sauti kama vile kanda, CD na DVD. Hivyo mtu au kampuni inapotaka kuweka kazi ya mtu katika kinasa sauti cha aina yoyote hulazimika kupata  ruksa kutoka kwa mwenye mali au taasisi ambayo ina mamalaka ya Mechanical Rights za kazi hiyo. Watunzi hupata Mechanical Rights kwa nyimbo zinaposambazwa na wauzaji.
Kama nilivyosema kabla ili kurahisisha ufuatiliaji na uratibu wa haki zilizotajwa hapo juu copyright collecting agency au copyright collecting society hutengenezwa ambapo aidha huwa ni chombo kilichobuniwa na watunzi au chombo kilichowekwa kisheria. Chombo hiki hupewa mamlaka na wanachama pia kutoa na kusimamia leseni mbalimbali kwa kazi walizozisajiri
Kwa hapa Tanzania Bara chombo ni COSOTA na Zanzibar COSOZA. Hivi ni vyombo vilichopewa mamlaka kisheria kushughulika kwa niaba ya watunzi kufuatilia haki zao, na kukusanya mafao yatokanayo na kazi hizo.
Kuweko kwa taratibu za kukusanya mirabaha kuna wapatia fulsa wanamuziki wakongwe kuendelea kupata chochote na hata kutajirika japo nyimbo zao ni za zamani, na pengine haziuziki tena. Mtunzi wa wimbo wa Red red wine alikwisha kata tamaa kimaisha uliporekodiwa upya wimbo huo ametajirika kutokana na wimbo huo.
Ni ukweli usiopingika kuwa kuna baadhi ya shughuli haziwezi kukamilika bila ya matumizi ya muziki. Kwa mfano biashara nyingi huongezea motisha kwa kupiga muziki. Mabaa, restaurant, magari ya kusafirisha abiria, na kadhalika. Haya ni matumizi makubwa tu ya muziki.
Shughuli mbali mbali za sherehe kama vile mikutano ya kisiasa, harusi birthday party hutawaliwa na muziki ambao matumizi yake huwa hayalipiwi kinyume kabisa cha haki za kimsingi za binadamu waliotunga nyimbo zinazotumika


Katika bendi, wimbo mali ya nani?

$
0
0

Kwa wafuatiliaji wa mambo ya muziki watakumbuka kuwa si mara moja ambapo kumekuweko na uvutano wa nani mwenye wimbo hasa pale ambapo mtunzi kwa sababu moja au nyingine kahama bendi. Nakumbuka niliwahi kuona kisanga hiki mara mbili wakati niko Vijana Jazz Band ambapo mara ya kwanza mwanamuziki mmoja ambaye alikuwa kaacha bendi siku nyingi alipoingia kwenye ukumbi akakuta bendi ikipiga wimbo ambao alitunga, akanza kupiga kelele kuwa bendi iache kupiga wimbo wake, kwani alikwishaacha bendi, tena aliacha kwa kufukuzwa. Japo kuwa Vijana Jazz ilikwisha kuurekodi wimbo huo kitambo. Mara ya pili pia ilitokana na mwana muziki mmoja ambaye yeye aliacha bendi kwa kupenda, kwani alisafiri kwenda nje ya nchi, na siku hiyo akaingia ukumbini na kukuta Vijana Jazz na Super matimila wakipiga pamoja. Vijana Jazz walikuwa wakipiga wimbo ambao yeye ndiye alitambulika kama mtunzi. Alichukua wireless mic kutoka kwa Dr Remmy na kuanza kutangaza kuwa wimbo unaoimbwa ni mali yake na kuanza kuimba katikati ya wimbo jambo lililozua ugomvi mkubwa na wanamuziki wengine wa Vijana Jazz wa kuanza kutukanana kwenye vipaza sauti. Sikinde nao walikuwa na ugomvi wakati Ramadhani Kinguti System alipoacha Bicco Stars na kuhamia Mlimani park Orchestra,  na ‘kuhama’ na wimbo wake.

Je, wimbo mali ya nani hasa? Katika bendi zetu nyingi, wimbo hutajwa kama mali ya mtunzi hasa wa maneno au mashahiri ya wimbo husika. Hivyo basi kuna watunzi huja na mashahiri peke yake au wengine mashahiri yenye sauti ‘melody’, na hata watunzi wengine hasa wapiga vyombo huja na wimbo wenye japo njia za chombo anachopiga kama ni kinanda au gitaa. Wimbo ukisha fika kwenye bendi, hapo huanza kuchangiwa na wanamuziki wote. Waimbaji watapanga sauti, na hata kubadili baadhi ya maneno, mpiga solo atatunga solo, mpiga bezi atatunga bezi mpiga kinanda atatunga kinanda alimuradi kiukweli wimbo huwa ni kazi ya watu kadhaa katika bendi. Kuna bendi ambazo ni mali ya mtu au kundi la watu ambao hugharamia vyombo vinavyotumika katika mazoezi, na kuwalipa hata mishahara wote walioko katika bendi, na hata wakati wimbo unatungwa , toka mtunzi mpaka wanamuziki wengine wote huwa katika ajira na hudai malipo kwa kufika katika mazoezi hayo. Akili ya kawaida tu inaonyesha kuwa wimbo uliokamilika si mali ya aliyeleta mashahiri peke yake, mwenye bendi anahusika, na wanamuziki wengine wengi wanahusika na kuufanya wimbo uwe ulivyo baada ya kukamilika. Sheria ya Hakimiliki ya Tanzania inasema ikiwa umeajiriwa na katika ajira yako ukatunga kazi, kama hakuna makubaliano tofauti na mwenye mali hiyo anakuwa muajiri. Ni vizuri wanamuziki waelewe hilo.

Kwa mfano katika wimbo ambao mwanamuziki aliukatisha kwa kutumia Microphone ya Dr Remmy, mwenyewe aliuleta ukiwa na beti mbili akiuuita Mama Sungura, jina ambalo lilikataliwa na wanamuziki wenzie mara moja, na wimbo ukatengenezwa vizuri na hatimae kuitwa Mama Chichi.

Mara nyingi wanamuziki huenda bendi mpya na kuendelea kupiga wimbo walioutunga zamani, hii huwezekana na katika malipo bendi yake ya zamani hulipwa kwa njia ya vyama vya hakimiliki kukusanya mirabaha kutoka kwenye sehemu ambazo hupiga muziki. Ila kurekodi ni lazima kuweko na makubaliano na bendi ya zamani hasa kama kinachokuja fanyika ni remix ya wimbo wa zamani.

MUNGU AWALAZE PEMA WALIOPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI HII

HAKI ZA MWANAMUZIKI KATIKA RINGTONE BADO NI UTATA MKUBWA

$
0
0
KUNA TATIZO KUBWA AMBALO LIPO KATIKA BIASHARA YA MATUMIZI YA MUZIKI KWA AJILI YA RINGTONES. KUNAUSIRI MKUBWA, TATIZO KUBWA NI WASANII WENYEWE KUTOKUWA NA MSIMAMO KATIKA HILI.
TAAARIFA HII ILIYOKO KATIKA GAZET YA CITIZEN NI USHAHIDI MKUBWA KUHUSU HILI. Soma HAPA 

Wasanii wanakula mizikiii kasimbaghooo

Wasanii watoa tangazo la kusitisha matumizi ya kazi zao

$
0
0
YAH: KUFUTA MIKATABA NA KUSIMAMISHA KUUZA MUZIKI WA BONGO FLEVA,GOSPEL,DANSI NA TAARABU KWENYE MITANDAO YA SIMU.
Husika na kichwa cha habari hapo juu,
Kwa ujumla wetu sisi Wasanii toka Tanzania tunaofanya muziki wa Gospel, Rhumba , Taarabu pamoja na Bongo fleva tumeamua kutoa agzio kwenu la kusimamisha mauzo ya kazi zetu za muziki katika mtindo wa Ringtone na Callertunes katika mitandao ya simu ya Vodacom, Zantel,Tigo na Airtel na kufuta mkataba tuliosaini kati yetu sisi Wasanii na Kampuni yako mpaka hapo tutakapokaa sisi kama wasanii, nyinyi kama wasambazaji wa muziki wetu, pamoja na Mitandao ya simu ili kuzungumzia namna mpya ya sisi na nyinyi tutakavyofanya kazi.
Sababu ya sisi Wasanii kusimamisha na kufuta mikataba kati yetu na wanaofanya biashara ya kuuza maudhui yetu ni pamoja kampuni husika kushindwa kuweka wazi taarifa za mauzo ya nyimbo pamoja na kutolipa katika muda husika kama ilivyoanishwa katika mikataba husika.
Sababu ya pili ni mitandao ya simu kuchukua kiasi kikubwa cha fedha ambacho ni asilimia themanini ya mauzo yote ya maudhui yetu, jambo hili linatuumiza na limetufanya tuendelee kuishi kwa kutegemea aina moja ya pato toka kwenye shoo.
Hivyo tumeziagiza kampuni zote zinazofanya kazi ya kuuza maudhui yetu kutoa maelekezo kwenye mtandao husika kuwaelekeza kusimamisha mauzo ya kazi zetu za sanaa ndani ya siku saba kuanzia leo tarehe 30/07/12 ikiwa pamoja na kusimamisha matangazo yote yanayotangaza mauzo ya kazi zetu kwa njia ya Television , Radio , blogs, website, Magazeti na Ujumbe Mfupi wa maneno mpaka hapo tutakapofikia muafaka.
Jumla ya wasanii 153 wameshasaini barua hizo na wengine wanaendelea kusaini.
Mwisho tunawashukuru kwa ushirikianao wenu, na tunaambatanisha sahihi zetu ili kuonyesha uthibitisho wa umoja wetu katika jambo hili.
Asante.
Viewing all 51 articles
Browse latest View live